Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

DHAMBI YA MAAGANO (LAANA YA UKOO) part 03

 inaendelea, sambamba na mwamdishi Late, Mwl. Godwin Dihigo. Je fundisho la kuridhi Dhambi wachungaji wamelipata wapi?   Uwenda pengine wachungaji wengi hawajaelewa fundisho lililopo katika Kuto 20: 4-6   Lakini hawajaelewa au khawataki kuwaambia ukweli washirika wao juu ya maana ya fundisho lililopo Kuto 20:5-6 katika mlango huo Mungu anasema Usijifanyie sanamu ya kuchonga wala mfano wa kitu chochote   kilichojuu mbinguni wala kilicho chini duniani wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia kwa kuwa mimi Bwana Mungu wako ni Mungu mwenye wivu nawapatiliza wana uovu wa Baba zao Kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao. Nami nawarehemu maelfu Elfu wanipendao na kuzishika amri zangu.   Manabii, wachungaji na Waalimu wa uongo uwafundisha kuwa watu wanaweza kurithi dhambi za Baba zao kwa sababu Mungu amesema anawapatiliza Watoto kizazi cha tatu mpaka kizazi cha nne kwa maovu ya Baba zao.   Kwa wale wasiochunguza maandik...

“Mwanga Wako Bado Unakuja: Hadithi Yako Haijaisha”

  "Nilifikiria kuwa ifikapo miaka 30 nitakuwa na biashara yangu kubwa, familia yangu, nyumba yangu ya ndoto… lakini sasa nipo 35, sina chochote. Nimechoka. Najiona nimechelewa.” Labda na wewe unajisemea hivi kila siku. Pengine kila jioni unatazama dari ukijilaumu, ukijilinganisha na wale mliomaliza shule pamoja ambao sasa wana magari yao, familia zao, au maisha mazuri ambayo wewe bado unayaota tu. “Nilizaliwa kwenye familia yenye shida, nimesoma kwa shida, nimesota kwa miaka mingi, na sasa naona miaka inasonga… na bado sijaona hata mwanga wa ndoto zangu. Yani Nimechelewa sana kufanikiwa!” Hapana ndugu yangu. Hujachelewa. Bado hujachelewa kabisa. Tumekuwa tukijiambia na kujiapiza mambo mengi sana, Lakini maisha hayana “ratiba ya darasani.” Maisha yana mitihani, majaribu, magumu, na changamoto zisizotarajiwa. Na kwa bahati mbaya, yanatokea hasa pale ambapo tulitarajia mwanga. Wengine wetu tumetoka kwenye familia masikini, hatukuwa na walimu wa kutufundisha maisha, hatuku...

Maumivu ya Moyo Ambayo Hakuna Anayeongelea.

Upendo ni moja ya hisia safi na zenye nguvu zaidi duniani. Ni hisia inayotuunganisha na wengine kwa undani wa kipekee, iwe kwa wazazi wetu, dada, kaka, marafiki, au wapenzi wetu wa karibu. Upendo unajenga daraja la imani, matumaini, usalama na heshima. Unapopendwa, unajihisi kuthaminiwa, kuwa salama, na kuwa nyumbani hata ukiwa mbali na kwenu. Lakini, ndani ya uzuri wa upendo, kuna upande wa pili, giza linalotanda pale unapovunjwa moyo. Maumivu ya mapenzi hayalingani na mengine. Ni kama mapigo ya moyo yanayokatika taratibu, unapoumia kimya kimya huku dunia ikiendelea kana kwamba hakuna kilichotokea. Na hakuna maumivu makali kama yale yanayotokana na kuvunjwa moyo na mtu uliyempenda kwa dhati yaani mume, mke, mchumba, mpenzi au rafiki wa karibu wa kimapenzi. Maumivu ya moyo hayaanzi tu pale mtu anapoondoka. Huanzia pale unapohisi kuwa hauko tena salama, unapojihisi kupuuzwa, kutojaliwa, au kudanganywa. Wakati mwingine, mtu anayekuumiza ni yule uliyemlinda zaidi, uliyemtambulisha kwa fam...

Kwa Nini Tunaogopa Kuwa Peke Yetu?

  "Upweke siyo laana, ni nafasi ya kuongea na nafsi yako kwa sauti ya ndani ambayo ulimwengu hauwezi kusikia." Zamani za kale, kabla ya kuwepo kwa magereza, jamii zilitumia adhabu za moja kwa moja kama kufukuzwa kwenye kijiji, kuchapwa viboko au hata kuuawa kwa makosa fulani. Lakini takribani miaka 3,000 iliyopita huko Mesopotamia (leo ni Iraq), ilibuniwa wazo la kwanza la kumtenga mtu kwa muda kama adhabu — gereza . Lengo halikuwa tu kumwadhibu, bali kumtenga , ili atafakari makosa yake na ajirekebishe. Katika karne ya 18, mfumo wa magereza ulianza kubadilika huko Ulaya na Amerika. Walianza kutumia "solitary confinement" yaani kumweka mfungwa peke yake kabisa bila kuzungumza na mtu yeyote kwa muda mrefu. Lengo lilikuwa kumlazimisha akutane na nafsi yake , akae kimya na kufikiri. Wanafikra wa wakati huo waliamini kuwa ukimya na upweke vina nguvu ya kumrekebisha mtu , lakini pia waligundua kuwa ndiyo adhabu kali zaidi kisaikolojia . Leo hii, hata bila kufun...