inaendelea, sambamba na mwamdishi Late, Mwl. Godwin Dihigo.
Je
fundisho la kuridhi Dhambi wachungaji wamelipata wapi?
Uwenda
pengine wachungaji wengi hawajaelewa fundisho lililopo katika Kuto 20: 4-6
Lakini
hawajaelewa au khawataki kuwaambia ukweli washirika wao juu ya maana ya
fundisho lililopo Kuto 20:5-6 katika mlango huo Mungu anasema
Usijifanyie
sanamu ya kuchonga wala mfano wa kitu chochote
kilichojuu mbinguni wala kilicho chini duniani wala kilicho majini chini
ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia kwa kuwa mimi Bwana Mungu wako ni Mungu
mwenye wivu nawapatiliza wana uovu wa Baba zao Kizazi cha tatu na cha nne cha
wanichukiao. Nami nawarehemu maelfu Elfu wanipendao na kuzishika amri zangu.
Manabii,
wachungaji na Waalimu wa uongo uwafundisha kuwa watu wanaweza kurithi dhambi za
Baba zao kwa sababu Mungu amesema anawapatiliza Watoto kizazi cha tatu mpaka
kizazi cha nne kwa maovu ya Baba zao.
Kwa
wale wasiochunguza maandiko kwao ni rahisi kuwaambia wachungaji wao sawa kabisa
pale wanapoambiwa wawe na maombi maalumu na sadaka maalumu kuondoa laana au
dhambi hiyo.
Nakata
ujuwe sasa.
Yapo
mambo mawili ya kuelewa katika mistali hii.
1. Mungu
anawapatiliza Watoto hao tu nao ni wale wanaomchukia Mungu katika maagizo yake
yaliyosema. Wale wanaowatii wazazi wao kwa kufanya dhambi kama zile wanazofanya
wazazi wao.
Kwa
mfano Baba anamwambia Mtoto wake lazima unywe pombe kama mimi ili nikifa wewe
utachukua urithi wa tabia zangu nk. Huyu Mtoto anapokubali kuchukua maovu yote
ya Baba yake anamchukia Mungu.
2. Hata
kama ilikuwa ndivyo ilivyokuwa Mungu aliwaambia Waislaeli atawapaliza wana uovu
wa Baba zao kizazi cha tatu na cha nne. Je mpaka leo ni kizazi cha ngapi tangu
aliposema?
Hii
ni kuonyesha kuwa wachungaji wengi wanawapoteza sana wanadamu wenzao.
Katika
2Nyak tunathibitisha hili kutoka katika Neno la Mungu. Tazama 2Nyak 25:1-4
maneno yanasema.
Amazia
alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala akatawala katika
Yerusalemu miaka ishirini na kenda na Jina la Mamaye aliitwa Yehoadan wa
Yerusalemu akafanya yaliyo ya adili machoni pa Bwana, lakini si kwa moyo
mkamilifu. Basi ikawa alipopata nguvu katika ufalme wake, akawaua wale
waliomuua mfalme Babaye. Lakini watoto wao hakuwaua ila alifanya sawa sawa na
hayo yaliyoandikwa katika Torati katika kitabu cha Musa kama Bwana alivyoamuru,
akisema: Mababu wasife kwa makosa ya wana wala wana wasife kwa makosa ya
Mababa. Lakini kila mtu atakufa kwa dhambi yake mwenyewe.
Swali
ambalo watu wangejiuliza.
Wamepata
wapi habari ya watu kurithi dhambi ya ukoo? Yaani mababu wametenda dhambi
watoto na wajukuu wakarithi dhambi zao?
Sijui
kama hii elimu ni ya kiroho kweli, Amazia anasema akawauwa wale watumishi wa mfalme
baba yake lakini watoto wao hakuwaua, kwa sababu Mungu amesema hakuna mtu
awezaye kurithi dhambi ya mtu mwingine.
Basi
hawa wasemao kuna dhambi ya ukoo ni watumishi wa shetani Mungu wa ulimwengu
huu.
itaendelea................
Maoni
Chapisha Maoni