Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Elimu

Shujaa Wetu wa Kila Siku Tunayemdharau na Kumchukulia Poa.

Kuna watu ambao kila siku wanainua mataifa bila kupanda jukwaani. Watu wanaojitoa, lakini hawatajwi. Watu waliojaa majeraha ya ukimya, lakini bado wanatabasamu. Leo, Palubongo tunakuletea hadithi ya shujaa tuliyemzoea sana kiasi cha kumsahau Mwalimu wa Shule ya Msingi. Asubuhi ya Maisha Yake Ni saa 11 alfajiri, kijiji cha Ng’ongo bado kimejaa giza. Ukisikiliza kwa makini, utasikia sauti ya sufuria ikigongana na jiko la mkaa. Mwalimu Rehema, mama wa watoto watatu, anapika uji wa mahindi kwa haraka kabla hajavaa kitenge chake cha bluu na kusafiri kwa miguu kilomita nne kwenda kufundisha darasa la pili. Barabarani, atakutana na maji ya mvua yaliyotuama, na wakati mwingine mbwa wa mtaani watamtisha. Lakini kila hatua anayoipiga, anaiona kama sala ya kimya kwa ndoto za watoto wake wa darasani. Anapoingia shule saa 1:30 asubuhi, hakuna chai, hakuna ofisi yenye kiyoyozi, hakuna kompyuta. Lakini kuna ubao, chaki, na watoto 72 waliokaa kwenye madawati yaliyopasuka, wakimsubiria s...

Mafunzo ya STEM Yaleta Mabadiliko kwa Walimu Nchini Tanzania

Imeandaliwa na Palubongo. M namo tarehe 24 na 25 Aprili, 2025, kituo cha Centre for Education and Lifelong Learning (CELL) kilicho chini ya Chuo Kikuu cha Aga Khan, kilifanya warsha (mafunzo) maalum ya kuwajengea uwezo walimu kutoka shule mbalimbali namna ya kufundisha masomo ya STEM (Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati) kwa ufanisi zaidi, kwa kutumia zana bunifu za kidijitali kama PhET Simulations . Warsha hiyo iliyofanyika katika kampasi ya Aga Khan iliyopo Upanga, Dar es Salaam, iliongozwa na Dkt. Esther Kibga, mtaalamu mahiri wa elimu ya STEM, akisaidiana na wawezeshaji wenzake Bi. Lucy Rweyemamu na Bi. Rose Iminza. Kwa muda wa siku mbili, walimu walishiriki katika mafunzo yenye shughuli shirikishi, majadiliano ya kina, na maonyesho ya mbinu mpya za ufundishaji wa STEM. Lengo kuu la warsha lilikuwa kuwawezesha walimu kuzielewa dhana za elimu ya STEM, kuzifasiri katika mazingira halisi ya darasani, na kuwasaidia wanafunzi wao kupata ujuzi wa karne ya 21 – ujuzi wa kufi...