Yapo Mambo mawili ya kufanya kabla ya
mahusiano (uchumba)
2. Kuwa katika uhalisia wako
“…Mimi
unielewe tu kuwa Nina wivu Sana, yani Sana tu sipendi kuona unatumia muda
mwingi na wengine. Ila najua nakupenda Kwa dhati ndio maana nakuwa hivyo. Nisamehe
pale ninapokosea.”
Kipindi
cha uchumba au kutafuta mwenza ni kipindi cha maandalizi ya maisha ya mapenzi
hasa ndoa. Ni kipindi ambacho jinsi ulivyo na namna unavyoenenda vitaweza
kumshawishi au kumvutia mtu kwako. Jambo kubwa linalokosewa kipindi hiki ni
kuigiza tabia au maisha fulani ili uonekane bora zaidi. Hali hii husababisha
kuwepo Kwa mahusiano yasiyo na uhalisia, mahusiano ya maigizo ambayo huunganisha
watu wawili wasio sahihi.
Kijana
aliye na imani na Mungu na anayeongoza maisha yake kwa msaada wa Mungu hawezi
kuigiza mwenendo wake wa maisha, unatakiwa kuwa wewe na uoneshe tabia zako na
misimamo yako ambayo umejiwekea katika maisha yako. Kama hupendi kuvaa nguo
ndefu basi kuwa hivyo, Kama hupendi kwenda club kuwa hivyo, Kama unapenda
kutoka mara kwa mara kuwa hivyo, kama hupendi kula chakula Fulani basi kuwa
hivyo ijulikane (ufunuo 3; 15-16).
Ukiwa katika uhalisia wako kipindi hiki itakusaidia kupata mtu sahihi ambaye
ataweza kukubaliana na tabia na mapungufu yako na wote kwa pamoja mtafanikiwa
katika maisha yenu. Ukiwa katika uhalisia wako itakusaidia kuwa na maisha
mepesi, hutatumia nguvu nyingi kuishi na mwenza wako kipindi cha uchumba hata
ndoa hapo baadae ambayo ndio paradise
inayotazamiwa. Kila mmoja akiwa katika uhalisia wake, itakuwa rahisi kujua
udhaifu wa mwenzi wake na ni vipi ataukamilisha udhaifu huo kwa ajili yake,
atatambua ni wapi nguvu ya mwenzi wake ilipo ili pia aweze kuitumia kukamilisha
mapungufu yake na kuleta mafanikio.
Ukiwa
katika uhalisia wako, utapunguza na kuondoa lawama zisizo na msingi katika
maisha yako na ya mwenzio, utajenga mahusiano bora ambayo msingi wake ni Mungu
na kweli. Ukiwa katika uhalisia wako utatambua mahali pa kuboresha pale
utakapoona nia na haja ya mabadiriko katika maisha yako, ukiwa wewe utampendeza
Mungu na kuzuia dhambi mbalimbali zinazotokana na udanganyifu. Lengo la
mahusiano ni kuandaa paradise ambayo ni
ndoa, mkiwa wakweli itakuwa rahisi kwenu wawili kuwa na pumziko la moyo.
Hutoweza kuwaza mabaya juu ya mwenzi wako kwakua unamfahamu alivyo, mambo anayoweza
na asiyoweza kufanya.
itaendelea.......
Maoni
Chapisha Maoni