Yapo Mambo mawili ya kufanya kabla ya mahusiano (uchumba).
1. Mungu kwanza
“Mungu
yu nami atanisaidia…. Mimi naamini maono yangu yatatimia tu ilimradi nayafanyia
kazi na nayaombea, yatatimia. Hata nikifa kesho ninauhakika utawaadithia watu kwamba
nilijitahidi kukuonesha upendo wa dhati…”
Mara
nyingi watu wanaishi Kwa mazoea nikimaanisha huishi kulingana na mazingira au
siku husika inavyotaka waishi. Ukiwa Kama mwanadamu aliyekamilika unapaswa kuwa
na ndoto, mawazo na mipango mbalimbali vitakavyo kusaidia kuishi vyema duniani.
Jambo moja ambalo linatakiwa kuwa katika mipango yako ni kuhusu mwenza wako,
unahitaji mwenza wa aina gani, kutoka familia gani, mwenye tabia gani n.k.
Hili jambo ni muhimu sana katika maisha
yako, ingawa utajiwekea orodha ya tabia, muonekano na chimbuko la mtu umtakaye
ila bado sisi ni wanadamu na tunaupeo wa kibinadamu. Pengine mawazo tuliyonayo
hayatatufaa baadae au tabia na matakwa tuliyojiwekea havitatukuza na kutupatia
maisha bora baadae hivyo tunamuhitaji Mungu kutusaidia katika maamuzi na
machaguo yaliyosahihi. (Mithali 9; 10).
Mungu wetu ni Mungu wa maarifa, Mungu mwenye hekima iliyozidi viumbe vyote. Mungu
hutuwazia mema kila siku na anatujua tangu tumboni mwa mama zetu. Katika mipango
yote tunayojiwekea mwenye kuikamilisha ni Mungu. (1wakorintho 2; 6-7).
Ukitaka
upate kile unachokihitaji lazima ujikite katika maombi kila wakati, maombi
yatakusaidia kuchambua vigezo ulivyo jiwekea na kuboresha zaidi. Mungu kupitia
maombi atakupa hekima ya kuchagua mwenza sahihi wa maisha yako, tujikite katika
kusali kila wakati, tumtangulize Mungu kwanza na kila kitu kitaenda sawa.
Hakuna muujiza
utakaotokea kama mtu kuibuka tu kwako bila mipango na maombi, yeye baba aliye
juu atakuwezesha kuchagua mtu sahihi kati ya wale wote utakaowaona kwenye
maisha yako. Wakati mwingine utaona umechagua mwenza ambaye ana tabia moja au
mbili tu au hana kabisa kati ya zile ulizojiwekea kama vigezo ila jua kama Mungu
akiwa ndani yako utakuwa mahali salama na umepata mtu sahihi.
Katika
wakati wa machaguzi unatakiwa kuwa mpole na usiyekuwa na haraka. Mungu wetu ni Mungu
wa ustadi, hakurupuki. Tumia muda wako vizuri katika kuchunguza upande wa pili
na kuvumbua kama kweli anakitu ndani yake ambacho Mungu anasema nawe katika
hilo. Binadamu tulio wengi tunatabia ya kuigiza tabia Fulani pale tunapohitaji
kitu, ukimshirikisha Mungu ukachukua muda utaweza kujua undani wa mtu na
umuhimu au ubora wake.
itaendelea......

Maoni
Chapisha Maoni