Na Samwel Dihigo.
Mahusiano
ya kimapenzi
Dhumuni langu sio
kuzungumzia mahusiano kwa ujumla bali ni kujikita katika mahusiano ya kimapenzi
ambayo kwa upana zaidi yamekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Katika
maisha yangu hapa duniani mpaka sasa nimeshuhudia watu wengi wakiteseka katika
aina hii ya uhusiano, wengine wamekufa, wengine hawana amani, wengine
wamepoteza nafasi kubwa sana n.k. Mahusiano ya kimapenzi yamekuwa chanzo cha
marumbano, uharifu, machukizo, vilio na visasi, mahusiano hayana tena upendo na
uimara kama hapo awali.
Kwa
kipindi hiki, mahusiano mengi yanaishia njiani na watu kufarakana, yale ambayo
yanapata nafasi ya kuwa hai basi yanakuja kufa kipindi cha ndoa na kufanya
maisha ya ndoa kuwa mabaya na kukera. Nimeshuhudia kwa ukubwa watu
wakiwalalamikia wenza wao kwenye ndoa na kuwashauri vijana kutothubutu kuolewa
au kuoa kwasababu ndoa zao zimekuwa kama jehanamu ya moto. Sisemi kwamba mimi ni
bora sana katika hili na ndio maana nimeamua kuandika hili la!, nimeamua
kufanya uchunguzi na kuja na majibu ambayo kwa upeo wangu naona yataweza
kusaidia katika kufumbua watu macho, kuwasaidia kuimarisha mahusiano yao na
kuwawezesha kufikia ndoa, si ndoa tuu bali ndoa yenye upendo na furaha, ndoa
tunayo ifananisha kama paradise au pepo.
Mahusiano
ya kimapenzi yapo katika hali mbili, moja ni uchumba na mbili ni ndoa. Katika
hali zote mbili kuna mambo muhimu ya kufanya ili kuimarisha kote, ndoa bora
inatokana na mahusiano bora ya uchumba ambayo yamefuata hatua kadhaa na kufanya
mambo kadhaa, na mambo hayo yanakwenda kuimarika zaidi kipindi cha ndoa.
Kutokana na hilo nimeona wazi katika kitabu hiki kuelezea mambo muhimu ya
kufanya au kuanza nayo kabla hujapata mwenza au kujiingiza katika mahusiano ya
kimapenzi na mtu, na ni mambo yapi ya kuyafanya baada ya kumpata mtu sahihi wa maisha
yako (uchumba), na kwa ujumla mambo yote hayo yatasaidia kuimarisha na
kutengeneza mahusiano bora na kuandaa ndoa njema hapo baadae ambayo ndio paradise tunayo itazamia. Ndoa haipaswi
kuwa kama jela au jehanamu ya moto, mahusiano au uchumba pia hayaitajiki kuwa
chanzo cha maumivu na majuto baina ya watu, watu wote kwa pamoja wakitimiza
wajibu wao basi watatengeneza mahusiano imara, bora, yenye furaha na ndoa njema
hapo baadae.
Kuna
mambo nane muhimu ya kufanya ili kufanikisha mahusiano mema ya kimapenzi baina
ya watu wawili, mambo hayo ni; Mungu kwanza, kuwa katika uhalisia wako,
mawasiliano, kujitoa, hudumia, usijilinganishe, upendo, mguso wa kimwili.
Ungana nami katika kuelezea mambo haya na naamini yatakwenda kukusaidia.
itaendelea.........
Maoni
Chapisha Maoni