Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambaye pia
ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Raisi wa Zanzibar Charles Hillary, amefariki
alfajiri ya leo 11 may, 2025 katika hospitali ya Mloganzila alikokuwa akipatiwa
matibabu.
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi,
Mhandisi Zena Ahmed Said, amethibitisha kifo cha ndugu Charles Hilary na kusema
kuwa “Marehemu Charles Hilary atakumbukwa kwa uzalendo wake, uadilifu na
mchango mkubwa alioutoa katika kusimamia mawasiliano ya Serikali kwa weledi na
ufanisi mkubwa”.
Ikimbukwe kuwa Charles Hilary alikuwa nguli wa habari na
miongoni mwa watangazaji bora wa Redio na Television nchini Tanzania na hata
nje ya Tanzania. Alifanya kazi kwenye vyombo vya habari vikubwa kama Radio one
na ITV, Azam TV na BBC London.
#palubongonews #palubongoblog

Maoni
Chapisha Maoni