JE MTU ANAWEZA KURITHI DHAMBI?
Kila
mkristo anapaswa kuiga mfano wa watu wa Beroya. Watu hawa wa Beroya Paulo
aliwasifu sana kwa hekima yao ya kutokuamini jambo bila kulichunguza. Hawakuona
kuwa ni busara kumuamini Paulo eti kwa sababu ni mtume bali waliyachunguza yale
asemayo kama yalikuwa sahihi.
Tunasoma
ukweli huo katika Matendo 17:10-12
Mara
hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya nao walipofika huko
wakaingia katika Sinagogi la Wayahudi. Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale
wa Thesalonike kwa kuwa waliyachunguza maandiko kila siku waone kwamba mambo
hayo ndivyo yalivyo. Basi wengi miongoni mwao wakaamini na wanawake wa Kiyunani
wenye cheo na wanaume si wachache.
Ukisoma
kwa makini mlango huu utagundua kuwa kuna watu wa aina mbili.
1. Wale
wa Thesalonike na
2. Wale
wa Beroya
Lakini
Paulo anawasifu watu wa Beroya kwa kuyachunguza maandiko. Si kila kitu
anachosema mwanadamu katika neno la Mungu ni ndiyo bila kupata ushahidi wa
biblia au neno la Mungu. Pata ushahidi muulize vizuri Yule anayekufundisha ili
ujiridhishe upate kushinda.
Watu
wa Thesalonike uwenda wako kama watu wa leo wanaopelekwa pelekwa kwa maneno ya
uongo kutoka kwa manabii wa uongo. Kwa sababu hawataki kusoma biblia pia
hawataki kufundishwa na waalimu waaminifu wa neno la Mungu kutoka kanisa la
Kristo. Waliamini waliyosema .
Mungu
anasema hakuna Mwanadamu yeyote anayeweza kurithi Dhambi ya mtu mwingine.
Katika
Ezekiel: 18:1- 4 tunasoma hivi:
Neno
la Bwana likanijia tena kusema je! Maana yake nini hata mkatumia mithali hii katika
Esraeli, mkisema Baba wamekula Zabibu mbichi nao watoto wakatiwa ganzi ya meno?
Kama mimi niishivyo asema Bwana Mungu hamtakuwa na sababu ya kutumia tena
mithali hii katika Israeli Tazama Roho zote ni mali yangu kama vile Roho ya
Baba ni mali yangu vivyo hivyo Roho ya Mwana mali yangu, Roho ile itendayo
Dhambi itakufa.
Katika
mstari wa 20 Mungu anaendelea kusema
Roho
itendayo Dhambi ndiyo itakayokufa Mwana hatauchukua uovu wa Baba yake wala Baba
hatauchukua uovu wa Mwanawe. Haki yake mwenye haki itakuwa juu yake na uovu
wake mwenye uovu utakuwa juu yake.
Je
kurithi Dhambi ya ukoo kunatokea wapi? Je hujagundua kuwa huo ni mpango wa
Wachungaji wa kujipatia fedha? Hayo tunayosoma hapo ni maneno ya Mungu
yaliyowaonya wanadamu wa wakati ule kuwa hakuna mtu awezaye kurithi Dhambi ya
mtu mwingine.
Mungu
akiendelea kusema, akamuagiza Musa awaambie wana wa Israeli juu ya watoto
kurithi zambi ya Wazazi wao si fundisho sahihi akasema hivi katika Kumb: 24:16
Mababa
wasiuawe kwa ajili ya Watoto wao, wala Watoto wasiuwawe kwa ajili ya Baba zao
kila mtu na auawe kwa Dhambi yake mwenyewe.
Maoni
Chapisha Maoni