Ruka hadi kwenye maudhui makuu

DHAMBI YA MAAGANO (LAANA YA UKOO) part 01


 Na late, Mwl. Godwin Dihigo.

Katika kitabu cha Muhubiri sura ya 7:29 tunasoma maneno haya;

“Tazama hili tu nimeliona, Mungu amemfanya mwanandamu mnyofu lakini wamebuni mavumbuzi mengi”

 

Sijawahi kusoma mahali popote katika biblia panaposema mtu aliyeokoka kweli kweli uwokovu uliyo sahihi anaweza kubaki na laana ya maagano ya ukoo.

 

Tena si yake yeye mwenyewe bali ya mababu na mabibi waliyoagana nayo zamani. Sijawahi kusoma maneno ya Mungu yanayosema mtoto anaweza kurithi dhambi ya baba na mama yake au niseme dhambi ya ukoo wao. Haya ni maneno ya kutegenezwa na wachungaji ili wajipatie faida.

 

Mungu alijua hili, ndiyo maana alituonya mapema

 

Tunasoma katika 2 Petro 2:1-3 maneno haya

“Lakini waliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu watakavyokuwako walimu wa uongo watakaoingiza kwa warevu, uzushi wa kupoteza wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. Na wengi watafuata ufisadi wao na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa ambao hukumu yao tangu zamani haikawii wala uvunjifu wao hausinzii”

 

Mungu anatujulisha kuwa fundisho la mkristo kupata laana ya ukoo ambao mababu na mababa waliagana na mizimu halina nafasi kwa wale wote waliookoka na kuwa ndani ya Yesu. Hawa ni manabii na walimu wa uongo, ambao kwa maneno yao ya kutunga ili wajipatie faida, hukumu yao haiko mbali.

 

Wale wote waliyo ndani ya Kristo, wale waliyookoka wokovu halisi usiyotungwa, Mungu anasema:

“Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya yakale yamepita, tazama yamekuwa mapya. 2 Kor 5:17.

 

Je wewe usomae ujumbe huu umeokoka wokovu halisi?, kama ndiyo hiyo dhambi ya ukoo nani ameibakiza ikiwa damu ya Yesu imekusafisha katika maji ya ubatizo?.

 

Wachungaji na waalimu wengi wanaofundisha fundisho hili hawakusoma kwamba hakuna mtu anayerithi dhambi ya mtu mwingine?. Nini kinachowasumbua hata wasiwaambie wanadamu wenzao ukweli?

 

Na hii yanadhihirisha maneno ya mungu katika kinywa cha mtumishi wake Paulo.  Mtume Paulo akiwaonya wakristo wa Rumi juu ya watu wajiitao manabii, wachungaji waliyojiita wenyewe na walimu wa uongo waletao mafundisho ya kutungwa akasema:

“Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu Rumi 16:18”.

 

Je umemuelewa vizuri Mungu kupitia mtumishi wake Paulo?, utapataje laana ya ukoo iwapo wewe umeokoka?, je huyo mwalimu wako na mchungaji wako bado unamwamini?

 

Mungu hakuongea hilo kwa warumi tu, bali alimtuma Paulo aseme na wafilipi waliyookoka. Tunasoma haya katika Filipi 3:18-20

“Maana wengi uenenda ambao nimewaambieni habari zao na sasa nawaambia hata kwa machozi kuwa ni adui wa msalaba wa kristo mwisho wao ni uharibifu, Mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedhaha yao waniao mambo ya duniani. Kwa maana sisi wenyeji wetu uko mbinguni”.

 

Mungu anasema watu wote waletao mafundisho ambayo Mungu hakuagiza, hawa wanafanya kazi ya Mungu wao wenyewe ambaye nitumbo.

 inaendelea................

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Maisha: Safari Yenye Maswali Zaidi Kuliko Majibu

  Karibu sana kwenye blogu yangu! Leo naandika chapisho langu la kwanza – mwanzo wa safari ya mawazo, mazungumzo, na tafakari juu ya maisha. Maisha ni safari isiyo na ramani kamili, na cha kushangaza ni kwamba kila hatua tunayopiga huibua maswali mapya. Tunazaliwa bila kujua lolote, tunaingizwa kwenye mifumo ya maisha – shule, kazi, mahusiano, jamii – tukitarajiwa kuelewa kila kitu kwa haraka. Lakini ukweli ni kwamba, wengi wetu tunaishi tukijaribu kuelewa maana halisi ya maisha, tukitafuta majibu kwenye imani, mapenzi, kazi, au hata burudani. 🔍  Kwa Nini Naandika Blogu Hii? Ninaamini kuwa kila mtu ana hadithi, swali, au wazo ambalo linaweza kumgusa mtu mwingine. Blogu hii ni mahali pa kuzungumza kuhusu yale mambo ya kila siku – yaliyo wazi, yaliyo magumu, na hata yale ya kushangaza ambayo hayasemwi sana. Tutazungumzia imani, mitindo ya maisha, afya, historia, burudani, mapenzi, na yale mambo ambayo huenda hujawahi kuyawaza kabisa. Lengo si kutoa majibu yote, bali kuibua f...

WIVINA SYLIDION: SHUJAA WA MABADILIKO KWA MSICHANA WA KITANZANIA.

 Na Palubongo Team. Katika kona ya kaskazini-magharibi mwa Tanzania, mji wa Bukoba unafahamika kwa mandhari yake ya kuvutia, ziwa Victoria, na watu wenye upendo. Lakini kuna jina moja linang’aa zaidi ya mandhari, jina la msichana kijana, mwenye ndoto kubwa, moyo wa dhati, na kiu isiyozimika ya kuleta mabadiliko: Miss Wivina Sylidion . Alizaliwa na kulelewa Bukoba, mkoa wa Kagera, Wivina alionyesha mapema kuwa safari yake haitakuwa ya kawaida. Akiwa na Shahada ya Sayansi na Elimu, aliamua kutumia elimu yake kama chombo cha ukombozi hasa kwa wasichana walioko kwenye mazingira magumu. Aliona mapema jinsi jamii inavyowatizama wasichana kama dhaifu, na akaapa kuwa sehemu ya mabadiliko hayo. Wivina si tu mwalimu wa darasani bali ni mwalimu wa maisha. Kupitia taasisi aliyoianzisha kwa moyo wake mwenyewe “Binti na Kesho Yako” , amekuwa akiwafikia wasichana mashuleni, akiwapa elimu ya afya, maarifa ya kijamii, stadi za maisha, na matumaini. Anaamini kuwa msichana anapojitambua, jamii ...

Pua: Kiungo Kidogo Chenye Nguvu Kubwa Kuliko Tunavyodhani

K una msemo wa Kiswahili usemao, "Usidharau kidogo chenye maana." Lakini kwa bahati mbaya, wengi wetu tumekuwa tukidharau kiungo kimoja cha mwili wetu kwa sababu tu ni kidogo – pua . Tunaizungumzia mara chache, hatuitunzi ipasavyo, na mara nyingine tunaificha au kuifanyia upasuaji kwa sababu hatuipendi jinsi ilivyo. Lakini hebu tusimame kidogo na tujiulize: je, tunafahamu kweli nguvu iliyo ndani ya kiungo hiki kidogo? Tuangalie pamoja nguvu ya pua; 1. Mlango wa Maisha: Kupumua Kila pumzi tunayovuta huanza kwenye pua. Hapo ndipo maisha huingia. Bila hewa, hakuna uhai. Lakini si tu kuvuta na kutoa hewa – pua huchuja vumbi, vijidudu, na hata unyevu wa hewa kabla haijafika kwenye mapafu. Ikiwa tungekosa pua, mapafu yetu yangekuwa kwenye hatari kubwa sana kila tunapopumua. 2. Hisia Zinazoamsha Kumbukumbu Hebu fikiria harufu ya chakula cha nyumbani – labda wali wa nazi, au samaki wa kupaka unaopikwa na mama. Au harufu ya mvua ya kwanza kunyesha ardhini. Au hata manukato ...