Oktoba 1991, jioni yenye
upepo mkavu, gari la kifahari lenye vioo vya giza lilisimama taratibu nje ya
kilabu maarufu cha warembo Dar es Salaam, kilabu kilichoitwa "Thompson Touch Club"
kilichoko Oysterbay. Ndani ya gari alikuwa mzee wa miaka 86, anayejulikana kwa
wengi kama Mzee Rashid Marshall mwinyimkuu,
tajiri wa mafuta aliyerudi Tanzania kutoka Marekani baada ya kujizolea
mabilioni ya pesa kupitia hisa na biashara za mafuta ya gesi huko Texas.
Hakuwa amezoea mazingira haya lakini aliamua kuingia tu kwa
kusindikizwa na kijana wake wa kazi. Ndani ya klabu hiyo, palikuwa na wasichana
waliovaa mavazi ya kuvutia, muziki wa Bongo Flava ukipiga taratibu, na harufu
ya perfume ghali ikijaa hewani. Mzee Rashid hakuwa amekuja kutafuta burudani, alikuja
kutuliza fikra, lakini bahati au mkosi ukaandika jambo jipya.
Pale mbele ya jukwaa, alimuona Nicole, msichana mwenye miaka 23 tu, anayefanya kazi ya
kucheza na kuhudumia wateja wakati wa mchana ili kujikimu. Hakuwa mrembo wa
kawaida. Alikuwa na sauti ya upole, uso wa huruma, na tabasamu la mtu ambaye
hajapewa nafasi ya kuishi ndoto zake.
"Ni wewe nimekuwa
nikikutafuta miaka yote hii?" Mzee Rashid alimnong’oneza siku
ya pili aliporudi tena Thompson Touch. Na kabla jua halijazama, alimkabidhi
bahasha yenye milioni mbili taslimu na ujumbe:
"Usirudi tena kazini.
kuanzia leo, ni Mimi na wewe. Mwanamke wa Maisha Yangu."
MAPENZI NA GHARAMA ZAKE
Ndani ya wiki chache, maisha ya Nicole yalibadilika, aliishi
kwenye jumba la kifahari huko Mbezi Beach, alipewa gari aina ya Mercedes Benz
nyekundu, safari za Ulaya, na zaidi ya shilingi milioni 500 zilitumika
kumnunulia vito vya thamani. Kila siku ilikuwa kama filamu ya mapenzi.
Lakini licha ya zawadi na maisha ya kifalme, changamoto
hazikukosekana. Mzee Rashid alikuwa mzee sana — afya yake ilikuwa dhaifu, mara
kwa mara alianguka bafuni, alihitaji uangalizi wa karibu, na mara nyingine alikuwa
mkali sana hasa usiku alipokuwa na presha au akimsahau Nicole kwa muda mfupi.
Ilikuwa ni mapenzi yaliyochanganyika na huduma ya uuguzi.
Nicole alipitia changamoto nyingi:
· Wivu wa jamii — walimuita
Malaya aliyeuza utu wake.
· Upweke wa kweli — marafiki
walimkwepa, wengi wakidhani amesahau asili yake.
· Shinikizo la familia ya Mzee — walimwona
kama mtu anayewinda urithi.
Lakini naye
alikuwa na upande wake wa furaha, alipendwa kweli kweli. Alipoanguka kihisia,
Mzee Rashid alikuwa akimwambia:
"Ningekuwa mdogo ningekuoa
siku ile ile. Umenifundisha kupenda hata wakati nalia."
NDOA NA MSIBA
Mwaka 1993
walifanya harusi ya kifahari kwenye hoteli ya Serena. Watu mashuhuri, viongozi
wa siasa, na wanamuziki maarufu walihudhuria. Magazeti yaliandika:
"Mrembo wa Strip
Club avishwa Pete na Bilionea!"
Lakini miezi 14 baadaye, mapenzi yao yaliingia kwenye historia.
Mzee Rashid alifariki ghafla baada ya kupata shambulio la moyo nyumbani. Nicole
alibaki akiwa mjane, kijana, tajiri, na peke yake.
Hapo ndipo vita halisi vilianza. Watoto wa Mzee walimfungulia kesi
mahakamani, wakidai ndoa ilikuwa ya kujipatia mali. Walitaka nicole afukuzwe,
achukuliwe kila kitu. Nyaraka za urithi zikapotea. Majumba yakazuiwa. Akaunti
za benki zikafungwa.
Alibaki na jina tu Nicole Mwinyimkuu.
HILI
NI BAHATI AU LAANA?
Je, kama ungekuwa wewe badala ya Nicole, ungefanya nini?
· Je, kupenda mzee kwa moyo au kwa maisha bora
ni dhambi?
· Je, ukijikuta
peke yako baada ya kupoteza aliyekupenda kweli, ni laana au sehemu ya bahati yenye mafunzo?
· Kama ni wewe,
ungetupa penzi kwa sababu ya umri
au ungetazama moyo wake?
Katika maisha ya leo, mapenzi, pesa, na bahati vimechanganywa kwa
viwango visivyoeleweka. Kuna wakati unaweza kukutana na mtu ambaye dunia
haitamuelewa, lakini yeye ndiye atakayekuinua juu. Kuna wakati unaweza kupata
vyote, gari, fedha, ndoa, umaarufu, lakini bado ukabaki mpweke rohoni.
Kama Nicole, unaweza kupendwa kweli lakini bado ukahukumiwa vibaya
na dunia.
Sasa swali linaendelea:
Je, unapopata vyote, pesa,
mapenzi, umaarufu na kisha ukapoteza ule moyo uliokupenda, ni Bahati au Laana?
Toa Maoni Yako Kwenye Komenti 👇👇👇
Ungekuwa wewe ni NICOLE, ungefanya nini?
Maoni
Chapisha Maoni