Jina langu ni Emma… Niliamini mapenzi yanaweza kuponya kila jeraha, kuleta furaha, na kunifanya nijisikie salama.
Nilikutana na
Franklin kwenye sherehe ya kumbukumbu ya siku y kuzaliwa ya rafiki yangu.
Alikuwa mkarimu, mwenye mzaha, baada ya kupeana namba za simu, kila asubuhi
alikuwa ananiamsha kwa mahaba na kiukweli alifanya hali ya hewa ya moyo wangu
kuwa ya kiutukufu.
Tulianza kuonana. Kunywa juice.
Kucheka bila sababu. Nikajikuta nimeanguka kwenye mapenzi.
Katika mahusiano yetu Siku moja alinijulisha
kuna mtu maalum sana kwake. Bestie wake. Anaitwa Jackline., akisema ni msichana
anayefahamiana naye kwa muda na ni marafiki tu wa karibu. Sikumpenda jackline
lakini hakuwai nipa sababu ya kuhisi kama kuna kitu kati yao.
Mara nyingi mpenzi wangu aliniaga na kusema:
"Baby niko kwa Jackline leo, tunapika
chapati na kusikiliza mziki. Huyu bestie wangu anakujua sana, kila kitu
anakutetea."
Niliamini. Kila mara alipokuwa kwa Jackline,
nilihisi wivu… lakini nikakumbuka, "Ni bestie tu."
Siku moja, nikiwa nyumbani kwa
Franklin, tulishinda pamoja nikafanya usafi wote wa nyumba yake, nikapika
tukala wote, kisha nikaondoka. Bahati mbaya nilisahau simu yangu. hivyo
Nilirudi usiku kuichukua bila kusema.
Niliingia kimya kimya kutaka kumshtua
mpenzi wangu kama utani. Milango ilikuwa wazi. Mziki wa taratibu ukisikika.
Nilifikiri amelala na kupitiwa
Lakini
kilichofuata… kilinivunja zaidi ya ajali yoyote.
Nilimwona… Franklin. Na Jackline. Sio
kwenye sahani ya chapati. Bali kwenye shuka walizojifunika pamoja.
Kwa hasira
nikamwita na kusema:
"Franklin…? Huu ni utani
gani…?"
Franklin kwa kutahamaki na hofu akajibu:
"Emma! Sio vile unavyofikiria…
Samahani"
Jackline kwa kutaka kuufunika ukweli akasema:
"Emma, si unajua ni bestie tu,
hii ni bahati mbaya…"
Nilianguka sakafuni. Machozi hayakuwa
tu ya uchungu… bali ya mshituko.
Niliamini mtu
mmoja… lakini alikua na moyo kwa wawili.
Jackline alikuwa
rafiki yangu pia. Baada ya kukutanishwa nae na mpenzi wangu franklin. Alikuwa mtu
wa karibu sana kwangu. Tulikuwa tukicheka pamoja,kuambiana siri zetu, kila kitu
kwa undani kabisa, tulikuwa tunafurahi na kupiga picha pamoja… na sasa, alikuwa
amepiga moyo wangu picha ya maumivu.
Sasa ni wiki tatu tangu niondoke
kwenye maisha ya Franklin.
Ninajifunza kupenda
bila kujiumiza. Kujua kuwa upendo sio kifo, sio kusamehe kila udhalimu kwa jina
la "mapenzi."
Lakini swali linabaki…
“Je, kweli kuna ‘bestie’ wa jinsia tofauti bila tamaa ya siri?”
Na kama mapenzi yalianza kwa uaminifu,
kwa nini yakome kwa usaliti?”
Je, umewahi kuumizwa kama Emma? Ungependa kushiriki hadithi yako? Tuandikie kwenye comment.
Na kama unataka kujifunza mengi kuhusu siri za mapenzi… subscribe sasa.
Maoni
Chapisha Maoni